Mbunge wa Kyadondo mashariki nchini Uganda Bobi Wine anatarajiwa kutangaza azma yake ya kuwania urais nchini humo 2021 wakati wowote kuanzia sasa.

Mwanamuziki huyo ambaye hivi majuzi alijiunga na siasa amethibitisha kwamba atampinga rais Miuseveni katika kinyang'anyiro cha urais kama mgombea huru na hivyobasi kumaliza uvumi uliokuwa ukienea kuhusu uamuzi wake.

''Tuliamua kwamba tutaupinga utawala huu'' , Bobi wine aliambia gazeti la Financial Times siku ya Jumatatu baada ya kuzungumza na shirika la habari la AP kwamba atawania urais.

Aliliambia gazeti la Financial Times kwamba zaidi ya wabunge 50 , ikiwemo 13 kutoka kwa chama tawala cha rais Museveni cha National Resistant Movement NRM waliunga mkono ugombeaji wake na hivyobasi kumpatia ujasiri wa kuogombea kiti hicho.