Msanii wa Rap kutoka kiwanda cha BongoFleva hapa nchini Billnass, amenyoosha maelezo kwa kile kinachoendelea katika mahusiano ya wasanii wenzake Nandy na Dogo Janja.

Billnass amefunguka hayo kupitia show ya Friday Night Live "FNL" ya East Africa Television, baada ya kuulizwa anajua nini kuhusu mahusiano na ukaribu wa Nandy na Dogo Janja.

"Kwa zamani mimi nimemkuta Dogo Janja na Nandy ni marafiki, kabla ya mimi kumfahamu Nandy tayari alikuwa na urafiki na Janjaro, kwahiyo sio mbaya hata wakiwa wapenzi kwa sababu hata Nandy sijui mahusiano yake na pia sijui kuhusu Dogo Janja, kwa hiyo hata wakiwa wapenzi ni vyema kwa sababu wote ni washkaji zangu, na sio wazo baya".

Aidha msanii huyo akaongeza kwa kusema kuwa yeye akiachana na mtu hawezi kumpangia au kutoa ruhusa ju ya mtu mwingine atakayetoka naye kwani watu wengi tu wanaishi na wapenzi wa zamani wa watu wengine na yeye hana donge wala wivu.

Ikumbukwe tu rapa Billnass na Nandy walikuwa katika mahusiano kipindi cha nyuma na pia zilishawahi kuvuja video na picha kwa wawili hao wakiwa faragha.