BAADA ya hivi karibuni baba wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Abdul Jumaa kunaswa live akiwa kimahaba msituni na msanii wa muziki na filamu za Kibongo, Baby Madaha, mama wa mwanamuziki huyo, Sanura Kassim ‘Sandra’ naye amemjibu, Ijumaa linakupa habari kamili.Mama Diamond au Mama D, mapema wiki hii alionekana kumjibu baba mtoto wake huyo baada ya kuachia picha zake kali akiwa kimahaba na mpenzi wake wa sasa, Shamte ambapo zilizua gumzo kama lote.Picha hizo zilisambaa kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram ambapo zinamuonesha mama Diamond na Shamte wakilishana keki kimahaba zaidi na watu wao wa karibu kushangazwa na mambo wanayoyafanya wazazi


hao kwani hayalingani na umri walio nao. “Jamani huyu mama naye amekuwa akijiachia mitandaoni kama vijana wa sasa hajui umri wake umeshapita, si awaachie vijana yaani hajishtukii kwamba hakuna wazazi wengine wa mastaa ambao wanafanya haya wanayoyafanya,” aliandika mmoja wa watu wao wa karibu waliokuwa wanatoa maoni kwenye picha hizo.Wiki iliyopita baba Diamond na Baby Madaha walinaswa kimahaba msituni wakati walipokuwa wamekwenda kufanya utafiti wa kazi zao katika Hifadhi ya Mazingira Asilia ya Magamba iliyopo wilayani Lushoto jijini Tanga ambapo picha zao zilisambaa kila kona.