Achilia mbali na zile kelele zilizopigwa na watu kutokea Afrika ya Mashariki kuhusu Album mpya aliyoiachia Beyonce ‘The Lion King: The Gift” iliyowashirikisha hasahasa wasanii kutokea Afrika Magharibi na wengi kudai kuwa hakufanya sawa kutokana na maneno mengi kuimbwa kwa lugha ya Kiswahili.

Sasa unaambiwa ukisikiliza ngoma ya ‘Brown Skin Girl’ inayopatikana kwenye Album hiyo aliyomshirikisha Wizkid pamoja na mwanae Blue Ivy, Beyonce amemtaja muigizaji Lupita Nyong’o na kumdondoshea sifa kibao ikiwemo kusifia uzuri wake pamoja na rangi ya ngozi yake kuwa nyeusi, Lupita alitoa shukrani zake za dhati na kusema “Asante Beyonce kwa hii zawadi”Beyonce hajamtaja Lupita tu amemtaja pia mume wake Jay Z kuwa ana asili kutokea Rwanda kwenye ngoma ya “Mood 4 Eva” inayopatikana kwenye Album hiyo hiyo ya ‘The Lion King: The Gift’ ambapo alisikika akiimba “My baby father, bloodline Rwanda”.