Wajasiriamali Wamachinga sasa kuanza kunufaika na mikopo ya kidijitali kutoka Benki ya CRDB kufuatia urasimishwaji wa kundi hilo uliofanywa na Serikali nchi nzima kupitia vitambulisho vya ujasirimali.

Akizungumza kuhusiana na fursa hiyo wakati wa Semina ya Wajasiriamali kwa Mkoa wa Morogoro iliyofunguliwa na Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Kebwe Steven, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela amesema huduma hiyo ya mikopo ambayo itapatikana kupitia mfumo wa SimAccount inalenga katika kuwajengea uwezo wajasiriamali wadogo nchini kukuza biashara zao.

“Mikopo hii itakuwa ikipatikana kwa mfumo wa kidijitali kupitia huduma yetu ya SimAccount, hii itawezesha wateja kupata mikopo kwa haraka zaidi kupitia simu zao za mkononi bila kutembelea tawini. Tunafanya hivi tukijua uhitaji wa mikopo kwa kundi hili la wateja ni mkubwa na mara nyingi wamekuwa na uhitaji wa haraka,” alisema Ndugu Nsekela.

Ndugu Nsekela alisema Benki ya CRDB imekuwa ikitoa kipaumbele kwa kundi la wajasiriamali katika mpango mkakati wake wa biashara ambapo benki imekuwa ikibuni huduma na bidhaa maalum kwa ajili ya kundi hilo ikiwemo mikopo. “Kwa mwaka jana pekee tumefanikiwa kutoa mikopo ya jumla ya shilingi bilioni 421.58 kwa wateja wetu wajasiriamali”, aliongezea Ndugu Nsekela.

Dkt. Kebwe ameipongeza Benki ya CRDB kwa hatua hiyo akisema hatua hiyo itasaidia kutimiza juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika kuwawezesha wajasiriamali wamachinga nchini kupiga hatua katika biashara zao ikiwa ni mkakati wa kuwainua kiuchumi kufikia Tanzania yenye uchumi wa kati.

Dkt. Kebwe alitumia fursa hiyo pia kuipongeza Benki ya CRDB kwa kuwa mstari wa mbele katika kukuza sekta ya kilimo nchini kupitia bidhaa yake ya FahariKilimo.

Dkt. Kebwe aliwataka wajasiriamali na wafanyabiashara waliohudhuria katika semina hiyo kuchangamkia fursa ya mikopo ya kilimo inayotolewa na Benki ya CRDB, huku akieleza kuwa mkoa wa Morogoro unafursa kubwa ya kimaendeleo kupitia sekta ya kilimo hususani kilimo cha miwa, mpunga, pamba, korosho na kahawa.

Mbali ya kupata mafunzo juu ya fursa mbalimbali za ukuzaji biashara kupitia huduma na bidhaa mbalimbali za Benki ya CRDB, Wajasiriamali hao pia walipata fursa ya kutoa maoni juu ya uboreshwaji wa huduma.

Hivi karibuni Benki ya CRDB imetoa kiasi cha dola za kimarekani 60,000 kudhamini tafiti ya kampuni bora 100 ikijikita katika kipengele cha wajasirimali ambacho ni muhimu katika maendeleo ya kiuchumi na kuchochea makampuni hayo kufanya vizuri zaidi.
Mkuuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Steven akisaliamiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela wakati alipowasili katika Semina ya Wajasiriamali iliyoandaliwa na Benki ya CRDB, katika hoteli ya Nasheera, Mkoani Morogoro, Julai 13, 2019. Katikati ni  Meya wa Manispaa ya Morogoro Pascal Kihanga. 
Mkuuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Steven akiwa ameongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela wakati alipoingia katika ukumbi tayari kwa Semina ya Wajasiriamali iliyoandaliwa na Benki ya CRDB, katika hoteli ya Nasheera, Mkoani Morogoro, Julai 13, 2019.
Mkuuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Steven akitoa hotuba yake wakati akifungua Semina maalum kwa Wajasiriamali iliyoandaliwa na Benki ya CRDB, , katika ukumbi wa hoteli ya Nasheera, Mkoani Morogoro, Julai 13, 2019.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akizungumza na wafanyabiashara wa mkoa wa Morogoro juu ya fursa mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo kwa wafanyabiashara katika Semina maalum kwa wajasiriamali iliyoandaliwa na benki hiyo iliyofanyika katika hoteli ya Nashera mkoani Morogoro, Julai 13, 2019. 
Meya wa Manispaa ya Morogoro Mh. Pascal Kianga akizungumza na wafanyabiashara wa mkoa wa Morogoro juu ya furs mbalimbali zinazotolewa na bench hiyo kwa wafanyabiashara katika Semina maalum kwa wajasiriamali iliyoandaliwa na benki hiyo iliyofanyika katika hoteli ya Nashera,