Na Khadija Seif, MichuziTV

BARAZA  la Sanaa la Taifa (BASATA) limewataka wasanii kufuata utaratibu wa kusajiliwa kwenye baraza hilo ili watambulike kwa mujibu wa sheria.

Hayo yamesema leo baada ya Wasanii Wa maigizo (Bongo Movie) Irene Uwoya na Steve Nyerere kutotambulika na BASATA kutokana na kushindwa kufuata utaratibu wa kisheria wa kusajiliwa.

Kaimu Katibu Mtendaji BASATA, Onesmo Kayanda  amesema kuwa kwa sasa wasanii wengi wanafanya kazi  zao za Sanaa bila ya kufuata taratibu za kujisajili.

"Wengi wanaingia katika sanaa bila utaratibu wanafanya kazi kwa ujanja ujanja mambo ya utandawazi pia yamekua yakichangia kutoona umuhimu wa kujisajili , badala yake linapotokea tatizo ndipo linapokuja swala la yeye kutotambulika na Basata,"

Kayanda amesema wasanii wengi  wanafanya kazi zao bila kutambulika na mamlaka husika zaidi mitandao ya kijamii ndiyo inawatambua zaidi na  anakua kinyume na kazi zake.

Aidha,Onesmo ameeeeza lengo la kuwaita wasanii hao wawili Irene uwoya pamoja na Steve Nyerere kufika Basata ni  kufanya mazungumzo kuhusu mambo ya tansia ya sanaa na  pamoja kupatiwa elimu,faida na hasara zitakazojitokeza endapo utakua unatambulika kisheria kama msanii kupitia Baraza la sanaa (BASATA).

" Tumezungumza mambo muhimu yanayohusu sanaa hichi ni kikao cha familia ndio kikubwa zaidi na tumegundua pia wao ni baadhi ya wasanii ambao hawajasajiliwa Basata na hawatambuliki kisheria.

Katibu huyo alifafanua Kitendo cha Msanii wa Bongomovie  Irene Uwoya kudhalilisha waandishi katika Mkutano wa Kampuni ya kuuza filamu mtandaoni ya Swahiliflix kilichofanyika katika ukumbi wa Kilimanjaro hotel  jijini Dar es salaam cha kuwarushia pesa wanandishi kwa dharau kuwa waandishi wasione limepuuzwa bali sio la kuliweka wazi sana kwa sasa.

"Tunatambua kuwa amefanya kosa sisi kama viongozi tunalifanyia kazi ila si lazima kuliweka wazi".