Mwimbaji nguli wa muziki wa injili nchini Tanzania amesimulia kisa chake ambacho alitakwa kimapenzi na baba mchungaji.

Akiongea na kituo cha redio mkoani Mbeya Bahati Bukuku amesema baada ya ndoa yake kuwa mashakani alimfuata mchungaji ambaye alimtisha kuwa haruhusiwi kuolewa bali asubiri mpaka kifo kiwatenganishe na mumewe. Bahati Bukuku anasema miaka mitatu baada ya ndoa yake hiyo kukumbwa na mtanziko mchungaji huyo alimpigia simu na kumtaka kimapenzi. Bahati alimjibu mchungaji huyo kuwa aendelee kusubiri maana bado kifo hakijamtenganisha na mumewe


Tazama Video: