MwanaMuziki maarufu visiwani zanzibar, Jamila abdalah ‘Baby J’ amefunguka kuwa anachokiamini ni kwamba dada wa msanii wa Bongo Fleva, nasibu abdul ‘Diamond’,Esma khan amebeba mzigo mkubwa sana wa dhambi, kutokana na sakata linaloendelea sasa hivi la kumuiba baba mtoto wake. Akizungumza na Za Motomoto, Baby J alisema anachosikitika ni kwamba Esma, amejibebea mzigo wa

dhambi usio na sababu kwa sababu anajua fika yule ni mwanaume wa mtu na tena ana mtoto mdogo. “Unajua kuna dhambi nyingine siyo hata za maana kabisa, kwa sababu Esma alijua wazi anachukua mwanaume ambaye ana mwanamke na mtoto juu lakini akafumba macho na kujifanya hajui kitu sasa huko si kujibebea dhambi zisizo za lazima kabisa,” alisema Baby J. Hivi karibu kuliibuka sakata zito la Esma kudaiwa kutembea na baba mtoto wa mwanamuziki Baby J na kuzua tafrani kubwa kwenye mitandao ya kijamii