MAMA wa Staa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, Bi Sandra maarufu kama Mama Dangote na mkwewe ambaye ni mpenzi wa Diamond, Tanasha Donna, wamefanya bonge la party pale Mlimani City wakisherehekea kumbukumbu ya siku yao ya kuzaliwa ‘birthday’ tarehe 7, Julai.Shughuli hiyo imehudhuriwa na mastaa kibao akiwemo Diamond mwenyewe na wasanii wa WCB ambao walipata nafasi ya kutumbuiza katika hafla hiyo ya kihistoria kwa familia ya Mama Dangote.Wakati akiingia ukumbini, Bi Sandra aliambatana na mumewe, Shamte, na mwanaye Diamond ambaye alikuwa na mpenzi wake, Tanasha Dona. Lakini sapraizi kubwa ilikuwa ni ile ya Baba Diamond, mzee Abdul Juma aliyetinga ukumbini hapo akiambatana na mkewe.Akipiga stori na Global TV Online kwenye red capet, Baba Diamond amesema alipelekewa kadi ya mwaliko wa sherehe hiyo na mwanaye wa kike ‘Queen Darleen’ wakati yeye akiwa safarini nchini Malawi lakini mwanaye Diamond alimsisitiza kuwa asikose kwenye hafla hiyo.Katika salam za pongezi, Baba Diamond amesema anamuombea mzazi mwenzake ‘Bi Sandra’ maisha marefu na Mwenyezi Mungu amwepusghe na balaa za aina yoyote huku akidai kuwa hajawahi kuonana na Tanasha uso ka uso wala kutambulishwa hivyo usiku huo ulikuwa muhimu kwake kumfahamu mkwe wake huyo ambaye kwa sasa tayari ana ujauzito wa Dianmomd.