Msanii AY amefunguka kuhusu stori za kuachana na mke wake, ambazo siku za hivi karibuni zilisambaa mtandaoni.

AY kupitia 5SELEKT ya East Africa Television amesema kuwa hizo ni stori za udaku na zitabaki kuwa hivyo tu.

 ''Hizo stori za udaku mimi nazitoleaje ufafanuzi, kwasababu mtu mmoja tu anaamka nakuandika anachotaka na muda mwingine unaweza hadi kujiangalia kwenye kioo kama ni wewe kweli''.

AY ambaye alikuwa ameambatana na Mwana FA pamoja na Christian Bella kutambulisha ngoma yao mpya walioshirikiana pamoja 'Pete'.

Kwa upande wao Bella na FA, wamesema kila mmoja alikuwa na ndoto ya kufanya ngoma na mwenzake na ilishatokea huko nyuma lakini ngoma hiyo hawakuimalizia na waliiacha kwa Producer Bob Junior.