Mfanyabiashara Khamis Luwongo (Meshack), anayetuhumiwa kumuua mkewe na kumchoma kwa magunia mawili ya mkaa, amepandishwa kizimbani kwa tuhuma za mauaji ya kukusudia.

Akisoma hati ya mashtaka Wakili wa Serikali Mwandamizi Wankyo Simon amedai leo mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi Salum Ally kuwa mshtakiwa anatuhumiwa kwa kosa moja la mauaji  kinyume cha Sheria ya kanuni ya adhabu namba 196 sura 16 kama kilochofanyiwa marejeo mwaka 2002.

Katika kesi hiyo ya mauaji namba 4 ya mwaka 2019, mshtakiwa Luwonga Mkazi wa Kigamboni, Dar es Salaam anadaiwa Mei 15,mwaka huu wa 2019 akiwa Gezaulole eneo la Kigamboni alimuua Naomi Marijani.

Mshtakiwa hakutakiwa kujibu lolote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.

Upelelezi wa kesi hiyo unaendelea ambapo mshtakiwa amepelekwa gerezani hadi Agosti 13, mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa.