MSANII wa Bongo Fleva, Lulu Euggen ‘Amber Lulu’ amefunguka kuwa pombe ndiyo imemharibia kila kitu na kumsababisha aonekane kituko kwenye jamii. Akizungumza na Ijumaa, Amber Lulu ambaye alifanya kituko kwenye Shindano la Miss Kinondoni,

lililofanyika wikiendi iliyopita baada ya kumtolea maneno machafu DJ wa siku hiyo kwa kumwambia wanashea ‘bwana’ ambapo alisema hayo yote yalitokana na ulevi hivyo mpaka sasa anajutia na ndiyo maana aliomba msamaha kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram.

“Unajua pombe inaweza kukuharibia kila kitu na ndivyo ilivyotokea kwangu, yaani imenifanya kwa sasa niichukie kwa sababu imenifanya kuwa kituko kwenye jamii yangu inayonizunguka kitu ambacho siyo kizuri,” alisema Amber Lulu