Baada ya mawaziri, George Simbachawene na Hussein Bashe kuapishwa asubuhi ya leo, Julai 22, 2019 na Rais Magufuli, Ikulu Jijini Dar es Salaam. Mbunge wa Mtama, Nape Moses Nnauye amewatumia salamu za pongezi viongozi hao.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Nape amesema kuwa uteuzi wa viongozi hao ni bora na kuwatakia mafanikio mema katika kazi yao mpya, huku akieleza sifa aliyoiacha Waziri aliyeondolewa katika nafasi yake, January Makamba.

"Uteuzi wa Mhe. Hussein Bashe na Mhe. Simbachawene ni katika teuzi bora kabisa. Ninawapongeza na kuwatakia majukumu mema!. Kaka January karibu 'back bench', hongera kwa utumishi wako!", amesema Nape.