Kiungo mshambuliaji wa Simba, Ibrahim Ajibu amesema kuwa hana hofu na kukosa namba kwani ushindani upo sehemu zote.

Ajibu amejiunga na Simba msimu huu akitokea Yanga kwa mkataba wa miaka miwili atapambana na viungo wengine ndani ya kikosi hicho wakiwemo Francis Kahata na Clatous Chama.

“Suala la ushindani wa namba mimi halinisumbui kwani hiyo ni kazi ya kocha kupanga kikosi, ninachojua mimi nimerejea nyumbani kikubwa ni kupambana ili kufanya vizuri,” amesema Ajibu.