Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe ameeleza kuwa miongoni mwa mambo yanayofanywa na Serikali ya awamu tano, ni Serikali hiyo kuwa na msimamo thabiti kwenye baadhi ya miradi ambayo imeamua kuitekeleza.


Zitto Kabwe amesema kuwa Serikali ya awamu ya 5 imekuwa na msimamo mkali kwenye miradi yake, toka imeanza kwenye bajeti ya kwanza mpaka bajeti ya nne.

"Kuna mradi wa reli, hela za ununuzi wa ndege kwenye bajeti ya pili na tatu fedha zimeongezeka, ukiendelea mtiririko kwenye bajeti ya kwanza mpaka ya nne tunayoijadili, utaona kwamba Serikali imetatua tatizo la kutokuwa na msimamo kwa hiyo hii ni chanya kwa Serikali." amesema Zitto

"Changamoto kubwa iliyopo miradi iliyamuliwa kutekelezwa na Serikali, miradi hii fedha zinaenda nje na haingizi fedha kwenye uchumi matokeo yake mzunguko wa fedha ni mdogo, na ndiyo maana ukuaji wa uchumi umekuwa ni mdogo." amesaema Zitto Kabwe.

"Pamoja na sisi wapinzani tumekuwa tukiwakosoa lakini hii chanya, kwamba mtu anaona acha ni feli, lakini ngoja nifanye ninachokiamini, hili ni tofauti sana na Serikali iliyopita" amesema Zitto Kabwe