Rapper Young Thug amegonga headlines kufuatia video clip iliyosambaa katika mitandao ya kijamii ikidaiwa ameamua kumpa mtoto wake mdogo gari aendeshe, wakati sio umri sahihi kuendesha gari kisheria na hatari kwa usalama wa mtoto mwenyewe.

Kufuatia mtandaoni kutawala kwa maneno maneno kuhusiana na kitendo hicho, vyanzo vya karibu kutoka kwa msanii huyo vimetetea na kusema kuwa binti wa msanii huyo aliyechini ya umri wa miaka 10 hakuwa pekeake kwenye gari alikuwa na mtu mzima na kitendo hicho kilidumu kwa sekunde 30 tu.Video iliyosambaa ikimuonesha binti huyo akiendesha gari huku akishika usukani kwa shida haikuwa na sauti lakini inatajwa kuwa mkono uliokuwa unashika usukani kumsaidia ulikuwa wa mwanamke na sio Young Thug mwenyewe, japo haijajulikana ni nani kwani video haikuwa na sauti ambayo ingesaidia kusaidia kuhisi.