Mkazi wa Mhunze wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Rafael Martine (34) anashikililiwa na Jeshi la polisi kwa Tuhuma ya kumuua Shija Mahoiga (45) mkazi wa kijiji cha Igaga kwa kutumia kipande cha chuma baada ya kumfumania akiwa amelala na mkewe.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga (ACP) Richard Awabwa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo limetokea june 21 majira saa tatu usiku nyumbani kwa Marehemu ambapo Rafael anatuhumumiwa kumshabulia kwa kumpika katika sehemu mbalimbali na kusababisha kifo.

Amefafanua kuwa chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi ambapo Rafaeli alivunja Mlango nyumba ya marehemu na kuanza kuwashambulia wawili hao hadi kusababisha kifo cha Marehemu huku mkewe aliyefahamika kwa jina la Maria Shija akiwa amelazwa katika hospitali ya wilaya ya kishapu kwa matibabu.

Kamanda Abwao ametoa wito kwa watu mkoani humo kutojichukulia sheria mkononi kwa kuheshimu sheria za nchi na na baada ya upelelezi mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.