Msanii wa Muziki kutoka lebo WCB, Queen Darleen amesema kuwa Wimbo wa Hamisa na Christian Bella Youtube umegota kwasababu Diamond katoa.

Darleen amesema kuwa Diamond katika kutoa kwake wimbo sio kwamba kamkomoa Hamisa na wala target yake haikuwa hivyo na wala hakuna aliyejua kama kuna mwenzake anachia Nyimbo.

"Wimbo wa Hamisa umegota Youtube kwasababu Diamond katoa wimbo na Diamond katika kutoa kwake wimbo sio kwamba kamkomoa, labda Hamisa ni target yake ilikuwa hivyo lakini unakumbuka Hamisa alikuwa hajatoa nyimbo Romy  Jones alikuja kucomment pale," alisema Darleen.

"Kwahiyo unakuja kuona tu vitu vinagongana lakini mwisho wa siku niliona Christian Bella alisema Viewers wamekwama."

Hivi karibuni Christian Bella na Hamisa Mobetto walitoa wimbo Mpya unaitwa 'Boss' ambayo unafanya vizuri kwenye mtandao wa Youtube