Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amewasili mjini Khartoum, Sudan, tayari kwa mazungumzo ya usuluhishi baina ya Baraza la Kijeshi na viongozi wa waandamanaji kufuatia ukandamizaji uliofanywa na jeshi wiki hii.

Äthiopien Sudan Premierminister Abiy Ahmed und General Abdel Fattah Al-Burhan Abdelrahman (Reuters/M. N. Abdallah)

Waziri Mkuu Ahmed aliwasili katika uwanja wa ndege wa Khartoum, na kuelekea moja kwa moja katika mazungumzo na majenerali wa Sudan ambao walimuondoa kiongozi wa muda mrefu Omar al-Bashir na kisha kuiongoza nchi. Baadaye, kiongozi huyo atafanya mazungumzo ya tofauti na viongozi wa waandamanaji.

Ziara yake inakuja siku moja baada ya Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa kusitisha ushiriki wa Sudan kutokana na mgogoro huo.

Hayo yakijiri shirika la afya duniani WHO katika taarifa yake limesema linatiwa wasiwasi na matokeo ya vurugu za hivi karibuni katika upatikanaji wa huduma za afya kwa watu wa Sudan.

Tarifa hiyo inasema hatua ya vikosi vya usalama kuvamia hospitali mjini Khartoum, ilisababisha huduma za dharura kusitishwa, wafanyakazi watano wa afya na wagonjwa kujeruhiwa pamoja na kuleta kitisho