warembo wakiwa katika picha ya pamoja na Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa uhifadhi Ziwa Manyara Noela Myonga ,na muhifadhi ujirani mwema Ibrahimu Ninga

Na Woinde Shizza, Arusha.

Warembo wanaowania taji la Miss Arusha 2019 wameaswa kuwa wahamasishaji na mabalozi katika kutangaza vivutio vya utalii vilivyoelekezwa hapa nchini .

Hayo yalisemwa na Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa uhifadhi Ziwa Manyara, Noela Myonga ambaye alikutana na warembo 16 wanaowania taji la Miss Arusha waliofika kutembelea hifadhi hiyo ya taifa ambapo aliwasihi wawe mabalozi katika kutangaza utalii .

Akizungumza na warembo hao, Myonga alisema urembo umebebwa na vigezo vingi ikiwa ni pamoja na kuwa na ufahamu wa mazingira uliopo pamoja na kujua vivutio mbalimbali vya utalii.

"Katika hifadhi hii Kuna vivutio vya kitalii ikiwa ni pamoja na Simba
wakweao miti ,makundi makubwa ya tembo na nyati, aina mbalimbali za ndege, bwawa la viboko, chemchem za maji Moto,ukuta wa bonde la ufa,Ziwa lenye mandhari ya kupendeza ambalo ni makazi ya makundi makubwa ya ndege aina ya heroe pia wingi wa aina za wanyama,alisema Myonga.

Noela alitoa shukurani kwa Kampuni ya Function House kwa kuruhusu warembo hao kufika katika hifadhi hiyo na aliwasihi waeendelee kutangaza utalii huu wa ndani.

Naye Meneja Itifaki wa Kampuni ya Function House Basili Elias alisema safari ya kutembelea vivutio vya utalii ilianzia katika hifadhi ya mkomazi na wameendelea kwa kutembelea hifadhi ya ziwa Manyara lengo ikiwa ni kuwawezesha washiriki kwa pamoja kwenda sambamba na kauli mbiu ya serikali ya kuhamasisha utalii .

"Sisi Kama waandaaji wa Miss Arusha 2919 tumeamua kuhamasisha utalii wa ndani na warembo hao ambao tunaimani watakuwa mabalozi wazuri kwani urembo si sanaa tu bali unagusa masuala mbalimbali ikiwemo uhamasishaji na kupata elimu ,"alisema Elias.

Shindano la Miss Arusha litafanyika julai 5 katika ukumbi wa Point Zone uliopo ndani ya Jiji la Arusha,