Baada ya Mbunge wa jimbo la Starehe nchini Kenya, Jaguar kukamatwa siku ya jana na jeshi la polisi nchini humo kwa tuhuma za uchochezi. Hatimaye baadhi ya wabunge nchini humo wameunga mkono kauli ya Jaguar huku wakitaka aachiwe huru kwani alichosema ndio mtazamo wa Wakenya waliowengi.



Akichangia maoni bungeni jana Juni 26, 2019, Mbunge wa Garissa mjini, Aden Duale amesema Jaguar alifanya jambo la kizalendo kwani Taifa hilo linahitaji kuwalinda wananchi wao kwenye masuala ya kibiashara.

Mbunge mwingine ni Moses Kuria wa jimbo la Gatundu Kusini, Amesema kuwa kauli ya Jaguar sio ngeni kwani viongozi wengi wa nchi hiyo walishawahi kuongea kuhusu wageni kupora fursa za kibiashara nchini humo.