Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
Teknolojia ya Mawasiliano inaweza kutumika kwa vijana katika kutatua changamoto ya ajira  pamoja na kusoma kozi mbalimbali katika Mitandao ya Simu za Mkononi.

Hayo yamebainishwa na Mratibu wa Mradi wa VISOMO katika Chuo VETA Kipawa  Charle's Mapuli wakati Maonesho yanayoendelea katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam amesema kupitia kusoma kwa kutumia mtandao baadhi wameweza kuhitimu katika kuunganisha mfumo wa Umeme viwandani.

Amesema baadhi ya vijana wameweza kujiunga kusoma katika mtandao na mwisho wa siku wamefanya vizuri katika kutengeneza mifumo mbalimbali ya Umeme. Mapuli amesema wanasoma katika Mitandao lakini mwisho wa siku mtihani wao ni kwa vitendo kufika chuoni na kuonyesha kile walichojifunza.

"Simu zinaweza kutumika katika kufanya maendeleo vijana wengi wanatumia simu janja lakini wanatumia kwa kufanya vitu ambavyo havina maendeleo na wale walitumia simu janja hizo wameweza kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Nae Meneja wa Mawasiliano VETA Sitta Peter amewataka wananchi kutembelea VETA kuangalia bidhaa mbalimbali wanazozalisha pamoja na kozi zinazotolewa na Vyuo vya VETA. Amesema katika kuelekea uchumi wa Viwanda VETA imejikita katika utoaji wa mafunzo kwa ajili Rasilmali itakayotumika katika Viwanda hivyo.

Peter amesema kuwa bila ya kuwa na Rasilmali yenye ujuzi malengo ya serikali yatakuwa hayajafikiwa kwa vitendo kama VETA itabaki nyuma.
 Meneja wa Mawasiliano wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Sitta Peter akizungumza na mteja aliyetembelea Banda la VETA katika Maonesho ya Sababa yanayofanyika katika Viwanja Vya Makini Julius Jijini Dar es Salaam.
 Mratibu wa Mradi wa VISOMO katika Chuo VETA Kipawa Charle's Mapuli akionesha sakiti ya Umeme viwandani uliotengezwa na vijana waliosoma katika Mtandao katika Chuo hicho katika Maonesho ya Sababa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Mwanafunzi wa Shule ya Watu Wenye Ulemavu Singida Abdi Kipara (34) akionesha umahiri wa ushonaji katika Maonesho ya Sababa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Zanura Hango (17) mwanafunzi wa Shule ya Watu Wenye Ulemavu Singida akionesha umahiri wa ufumaji vitambaa katika Banda la VETA katika Maonesho ya Sababa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam.