Vanessa Mdee Akiri Kuachana Na Jux (PICHA)
Mwimbaji wa Bongo Fleva Vanessa Mdee ametangaza rasmi kupitia Instagram story yake kuwa ameachana na aliyekuwa mpenzi wake Juma Jux baada ya shabiki kuuliza kama hakuna mapenzi tena kati yake na Jux.
Vanessa Mdee alijibu ‘Ndio, lakini ni marafiki wazuri sana na tutabaki kuwa familia daima’ swali hilo limekua likionekana kutojibiwa mara nyingi endapo wawili hao wakiulizwa kuhusu penzi lao kuvunjika, siku kadhaa zilizopita Mimi Mars ambaye ni mdogo wake Vanessa aliweka wazi kuwa Jma na Vee wameachana na wamebaki kama marafiki.
Juma Jux pamoja na Vanessa walianza mahusiano yao miaka kadhaa iliyopita na August 2017 walitengana lakini ndani ya mwaka huo huo wa 2017 walirudiana rasmi juu ya stage kwenye tamasha la Fiesta lilofanyika Dar Es Salaam.