Rais wa Uturuki Reccep Tayyep Erdogan amesema kuwa ana matumaini kwamba mfumo wa kujilinda dhidi ya makombora wa Urusi ambao Washington unauona kama tishio kwa ndege za Marekani utawasilishwa nchini humo mwezi Julai.

Marekani imesema kuwa Uturuki haiwezi kuwa na mfumo huo wa S-400 pamoja na ndege za kivita za Marekani aina ya F-35.

Lakini bwana Erdogan amesema kuwa Uturuki itamwajibisha mtu yeyote atakayeiondoa kutoka kwa mpango huo wa ununuzi wa ndege za F-35.

Uturuki ambayo ni mwanachama wa Nato imetia asaini ya kununua ndege 100 aina ya F-35 na imewekeza vya kutosha katika mpango huo wa F-35.

Kampuni za Uturuki huzalisha vipande 937 za ndege hizo.

Bwana Edogan alisema kuwa anatumai kutatua hali hiyo na Marekani kupitia njia za kidiplomasia kabla ya mktano na rais Trump mwisho wa mwezi Juni, kulingana na chombo cha habari cha Reuters.

Uturuki imekuwa ikipigania sera ya ulinzi ya kuwa huru na imeimarisha uhusiano wake na Urusi kufuatia kuharibika kwa uhusiano wake na Marekani pamoja na mataifa ya Ulya.

Je Markani imekuwa ikiiambia nini Uturuki?
Kaimu waziri wa ulinzi nchini Marekani Patrick Shanahan wiki iliopita aliiandikia Uturuki kwamba Marekani imesikitishwa kusikia kwamba wanajshi wa Uuruki wametumwa Urusi kujifunza mfumo huo wa S-400

Afisa mwengine mwandamizi kutoka Marekani katika wizara ya ulinzi Ellen Lord, aliambia maripota kwamba Marekani haikutaka maafisa wa kiufundi wa Urusi kuweza kuona udhaifu wa F-35.

Maafia wa Marekani badala yake walikuwa wakitaka Uturuki kununua mfumo wake kujilinda dhidi ya makombora wa Patriotic Missile.

Uturuki ina jeshi la pili kwa ukubwa katika Nato, muungano wa kijshi wa mataifa 29 ulioanzishwa kujilinda dhidi ya kile kilichoitwa kuwa Muungano wa Soveiti wakati huo.