Bondia maarufu kutoka Uingereza, Tyson Furry alfajiri ya kuamkia jana alimtwanga KO bondia kutoka Ujerumani, Tom Schwarz kwenye mchezo wa uzito wa juu.

Mchezo huo usiokuwa wa ubingwa umepigwa katika ukumbi wa MGM Grand, Las Vegas, Marekani ambapo Tyson alimpiga KO mbabe huyo kwenye raundi ya pili ya pambano hilo lililokuwa na raundi 12.

Kabla ya kupoteza pambano la hilo, Shwarz alikuwa na rekodi ya kushinda mapambano yote aliyowahi kushiriki, ameshinda 24 (KO 16).

Baada ya pambano hilo, Tyson Furry amethibitisha kuwa mwezi Oktoba watarudia pambano na mbabe Deontay Wilder huku akimchimba mkwara mzito. Kwenye pambano la kwanza lisilo la ubingwa, lililopigwa mwezi Machi mwaka huu, Tyson Furry alitoka sare na Deontay Wilder.