Wakati akiwa katika wakati mgumu kutokana na kupata majeraha ya kifundo cha mguu na kuondolewa katika michuano ya Copa America, Neymar anazidi kuingia katika wakati mgumu kutokana na kashfa yake ya ubakaji kuzidi kushika kasi na kuchukua sura mpya.

Imeripotiwa kuwa Polisi nchini Brazil wamemuita Neymar na kumuhoji kwa saa tano ili kubahini ukweli wa tuhuma dhidi yake, pamoja na kuwa Neymar aliwahi kutumia ukurasa wake wa instagram kujisafisha na kukanusha tuhuma dhidi yake ila mambo yanazidi kuwa makubwa zaidi.

Neymar amefanyiwa mahojiano hayo kwa saa tano baada ya kuwa na kesi yenye tuhuma za ubakaji akiwa nchini Ufaransa Paris mwezi uliopita katika hotel, mwanamke anayedaiwa kuwa nae Neymar inaelezwa kuwa walikutana nae mtandaoni