RaisTrump amesema kuwa hataki vita lakini akaionya Iran kuwa itakabiliwa na makosa ya "uharibifu" vita vikizuka.

Akizungumza na kituo cha habari cha NBC siku ya Ijumaa, alisema Marekani iko tayari kwa mazungumzo lakini haitakubali Iran kutengeneza silaha za nyuklia

Pia alizungumzia kwa kina kwanini alisitisha mashambulizi dhidi ya Iran dakika za mwisho kujibu hatua ya taifa hilo kudungua ndege yake isokuwa na rubani wiki hii, akisema aliambiawa raia 150 wa Iran wangeliuawa.Tehran Inasema ndege ya Marekani ambayo haikuwa na rubani iliingia anga lake mapema siku ya Alhamisi. Marekani inasisitiza kuwa ndge hiyo ilikuwa ikipaa juu ya anga la kimataifa.

Hali ya taharuki imekuwa ikiongezeka kati ya mataifa hayo mawili, huku Marekani ikiilaumu Irankwa kushambulia meli za mafuta zinazohudumu katika eneo hilo.