RAIS wa Marekani, Donald Trump,  amezindua kampeni zake kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 ambapo ameuthibitishia umma wa Wamarekani kuwa mwaka 2020 atagombea tena nafasi hiyo ya urais licha kupingwa sana na baadhi ya wanasiasa na raia wa taifa hilo.Katika hotuba yake Trump amegusia masuala ya utoaji mimba, familia, umiliki silaha, na ukuaji wa uchumi wa taifa hilo na kueleza kuwa 2020 asipochaguliwa hali itakuwa mbaya zaidi.Kwa sasa Trump anapingwa vikali na baadhi ya raia na wanasiasa wa taifa hilo lakini yeye mwenyewe ameuthibitishia umma kuwa atagombea.