Mchezaji wa Leicester City na Uingereza Harry Maguire, 26, anatarajiwa kuwa beki ghali zaidi duniani wiki hii wakati atakapojiunga na Manchester City kwa dau la £80m baada ya kukataa kujiunga na Manchester United. (Mirror)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu hii, Maguire kuwa beki ghali zaidi dunia, Liver na United zapigana vikumbo kwa kinda wa Real Betis, Firpo

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu hii, Maguire kuwa beki ghali zaidi dunia, Liver na United zapigana vikumbo kwa kinda wa Real Betis, Firpo

Liverpool na Manchester United watapigania saini ya mchezaji wa Uhispania na Real Betis beki wa kushoto Junior Firpo, 22. (Marca)
Manchester United watatumia kifungo cha sheria ya kumuongezea miezi 12 Marcus Rashford katika kandarasi yake uku kukiwa na hofu kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 huenda akaondoka man United wakati mkataba wake utakapokamilika mwisho wa msimu ujao. (Sun)