Times FM redio, inasikitika kutangaza kifo cha Mwanafamilia wao DJ Rguy kilichotokea usiku wa kuamkia leo akiwa kwenye majukumu yake ya kawaida nje ya kazi.Hii ndio taarifa iliyotolewa na kituo cha Times FM kuhusiana na msiba huo;

"Ndugu zetu.. Wanafamilia ya Radio Times tunasikitika kutangaza Kifo cha Mwanafamilia Mwenzetu na Dj. Wetu EMMANUEL JULIUS MAGIGE maarufu kama DJ Rguy."

"Dj wa Siku nyingi aliyeacha Alama na Heshima ya Burudani ya Muziki (anafahamika kuwa Dj. wa Kwanza Nchini kupiga Nyimbo za Kiafrika zaidi). R Guy ametuaga Usiku wa kuamkia leo tarehe 8 Juni, 2019 akiwa kwenye Majukumu yake ya kawaida nje ya kazi."

Tutaendelea kuwapa taarifa na utaratibu zaidi kadri muda unavyokwenda. Mwenyezi Mungu ampumzishe pahala pema. Amiin.!