Anaandika Abdullatif Yunus, wa Michuzi TV
Shirika la Umeme Nchini Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Kagera limefanya oparesheni ya kushtukiza katika Halmshauri ya Wilaya ya Bukoba na kubaini ubadhilifu na wizi wa umeme unaopelekea hasara kubwa ya upotevu wa umeme, ikiwemo uhalibifu wa miundo mbinu ya shirika hilo.
Ziara hiyo ya kushtukiza ilyofanyika mnamo Juni 17, 2019 ikongozwa na Afisa Usalama wa Shirika la Tanesco Mkoa wa Kagera Bwana Steven Maganga imefanikiwa kubaini wafanyabiashara wa senene katika kijiji cha Ngarama Kata Katoro wakiwa wamejiunganishia umeme kwa njia zisizo halali hali hiyo ikiwa ni uhujumu wa Shirika la TANESCO na kurudisha nyuma Jitihada za maendeleo ya Nchi.
Wizi huo wa umeme katika kijiji hicho unasababishwa na biashara ya senene ambapo biashara hiyo hutumia umeme mkubwa ikiwa taa moja ya umeme hutumia KW 200 – 300, na kwa mfanyabiashara mmoja hufunga taa zaidi ya tano, na kupelekea mita kuzidiwa na kuungua hivyo njia pekee inayofuata kwa wafanyabiashara hao ni kujiunganishia umeme moja kwa moja kutoka kwenye nguzo za umeme wa TANESCO.
Akizungumza katika eneo la tukio Afisa Usalama wa Tanesco Bwn. Maganga amesema kuwa kufuatia wizi huo shirika limeanza kuchukua hatua za makusudi mara moja kwa kushirikiana na serikali ya kijiji kwa kuwastishia huduma wateja hao wasiokuwa waaminifu kwa kung’oa mita zao huku akitoa angalizo endapo hujuma hizo zitaendelea Shirika litakuwa tayari kung’oa hadi nguzo na kukiacha kijiji chote gizani.
Katika hali ya kushangaza wakazi wa maeneo husika wameonekana kukimbia maeneo yao na kuziacha nyumba zikiwa zimefungwa, kana kwamba hamna shughuli yoyote inayoendelea kijijini hapo, ilihali Miongoni mwa waliokamatwa katika msako huo ni pamoja na Ndugu aliyekiri kuunganishiwa umeme wa wizi na mmoja kati ya Vishoka (jina limehifadhiwa) ambaye inadaiwa aliwahi kuwa mtumishi wa Shirika la Tanesco siku za nyuma kisha kutimuliwa, huku majina ya wote waliobanika katika wizi huo yakifikishwa katika kituo kidogo cha Polisi Kijijini hapo, baada ya kusitishiwa huduma hiyo ya Umeme.
Pichani shughuli ya kung'oa Mita na kukata huduma ya umeme ikiendelea Kwa waliobainika kuhujumu shirika la Umeme Mkoani Kagera, kijiji Cha Ngarama Kata Katoro Wilayani Bukoba.
Pichani ni Baadhi ya Mita zilizoungua baada ya kulemewa mzigo Wa Taa za Senene ambazo hufungwa Kwa ajili ya kutega na kuvuna Senene maeneo ya Katoro Bukoba.
Pichani ni baadhi ya nyumba za wateja Wa Tanesco ambao sio waaminifu, baada ya kugundua ujio Wa Tanesco mahala hapo walifunga nyumba zao na kuingia mitini.
Pichani shughuli ya kung'oa Mita na kukata huduma ya umeme ikiendelea Kwa waliobainika kuhujumu shirika la Umeme Mkoani Kagera, kijiji Cha Ngarama Kata Katoro Wilayani Bukoba.
Pichani ni namna wafanyabiashara wanavyotumia njia hii kuvuna Senene wakati Wa usiku ambapo huwasha Umeme na kisha Senene hupumbazwa na mwanga mkali na kudondoka kiurahisi katika bati hizo
Shughuli ya Kubaini Mita zilizofanyiwa hujuma ikiendelea chini ya Maafsa wa Tanesco na Uongozi Wa Kijiji Ngarama Kata Katoro Wilayani Bukoba.