Kikosi cha Taifa Stars kimpoteza tena mchezo wa Kombe la Mataifa ya Afrika awamu hii dhidi ya Kenya kwa kuchapwa mabao 3-2.

Kipigo hiki kimekuwa cha pili baada ya mechi ya kwanza kufungwa mabao 2-0 na Senegal.

Mabao ya Kenya yamefungwa na Michael Olunga aliyeingia kambani mara mbili huku moja likiwekwa kambani na Johanna Omolo.

Taifa Stars imefunga mabao yake kupitia kwa Mbwana Samatta na Simon Msuva.