Kama wewe ni shabiki wa Muigizaji mkongwe wa filamu nchini Marekani, Sylvester ‘RAMBO’ Stallone na upo Uingereza na ungehitaji kupiga naye picha kwenye tamasha lake la mitindo litakalofanyika nchini humo. Basi utatozwa Euro 849 sawa na Tsh Milioni 2 ili uweze kupiga naye picha.


Sylvester Stallone
Muigizaji huyo atakuwa na matamasha ya mitindo nchini humo kwenye majijini ya London, Manchester na Birmingham na yanatarajiwa kufanyika kati ya  mwezi Agosti na Septemba mwaka huu.

Wakati ukishangaa gharama za kupiga picha na mkongwe huyo, Pia viingilio vya kwenye matamasha hayo ya UK Events zinauzwa pauni 125 hadi 325 sawa na Shilingi 365,ooo/- na 950,oo/- za Kitanzania.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Mail, Rambo mwenye miaka 72 ameeleza kuwa waandaaji wa matamasha hayo wametaja hiyo kama njia ya kupunguza msongamano wa kupiga picha na kuongeza kipato mbali na viingilio.