Spika wa Bunge Job Ndugai amemuomba Waziri mkuu kumruhusu Waziri na Michezo Harrison Mwakyembe na Naibu na Waziri Juliana Shonza kuelekea nchini Misri kwa ajili ya kuiunga mkono timu ya Taifa ya Tanzania.


Kauli hiyo ya Spika Ndugai imekuja ikiwa ni siku chache baada ya baadhi ya Wabunge zaidi ya 48 ambao walikwenda nchini Misri kwa ajili ya kuiunga mkono timu ya taifa ya Tanzania kurejea nchini jana.

"Wote kama Bunge tuna uchungu na nchi yetu na vijana wetu, tumuombe Waziri Mkuu kama Waziri wa Michezo na Naibu watendelea kuwa hapa wakati timu iko Misri haitakuwa picha nzuri, hili jambo ni la kitaifa, na linagusa wengi mno." amesema Spika Ndugai.

Kwa upande wake waziri wa michezo Dk. Harrison Mwakyembe amejitetea kwa kusema alibaki kuweka badhi ya mambo sawa yanayohusiana na timu hiyo,

Katika mechi ya ufunguzi taifa stars ilifungwa magoli mawili kwa sifuri dhidi ya wazoefu Senegal ambapo itacheza mechi ya pili dhidi ya kenya alhamisi na wabunge zaidi ya 30 wanaondoka kesho kwa ajili ya kuishangilia timu hiyo.