*Wahaidi kuendelea kushiriki katika sekta hiyo na kuwaomba wadau wengi zaidi kujitokeza katika kuboresha zaidi mazingira ya ujifunzaji kwa wanafunzi ili waweze kufikia malengo yao 

SHIRIKA la SOS Children Villages kwa kushirikiana na Taasisi ya Patel Brotherhood  wamekabidhi vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Chanika ikiwa ni mwendelezo wa kuinua sekta ya elimu hasa katika masuala miundombinu na vitendea kazi. 

Akizungumza katika hafla hiyo ya makabidhiano Meneja mradi kutoka Shirika la  SOS Children Villages  Elamu Mkayange amesema kuwa katika miradi inatekelezwa na Shirika ilo ni kusaidia katika sekta ya elimu, na katika mradi huo wamefanya ukarabati wa madarasa 11 ambayo yamegharimu shilingi milioni 80, pamoja na vitabu 150 na shule 10 kutoka Chanika zipo katika mpango wa kupewa vitabu.

Amesema kuwa hadi sasa wamejenga maktaba 2 na vyoo katika shule zilizopo kata za Chanika na Zingiziwa huku akieleza kuwa wamelenga zaidi ya watoto 2000 ambao watafurahia maisha katika sekta ya elimu, amesema kuwa zaidi ya Bilioni 1.8 zimetengwa ili kuendeleza sekta ya elimu katika kata za Chanika na Zingiziwa na ameiomba Serikali na wadau mbalimbali kujitokeza na kusaisia sekta hiyo muhimu.

Kwa upande wake msemaji wa taasisi ya Patel Brotherhood Anil Patel amesema kuwa lengo la kutoa kusaidia sekta hiyo ni kuinua sekta ya elimu kwa kuweka mazingira rafiki wa wanafunzi ili waweze kutimiza ndoto zao.

Amesema kuwa wataendelea kuchangia vitendea kazi hasa vitabu na miundombinu ili watoto waweze kutimiza ndoto zao.

Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Chanika Ladislaus  Mutanda amesema kuwa wamekuwa n changamoto ya madarasa katika kata ya Chanika na hiyo ni kutokana na uhamiaji wa makazi mapya katika maeneo hayo, hivyo madarasa bado hayatoshelezi.

Mutanda ameiomba wizara ya Elimu kuangalia suala hilo la upungufu wa madarasa ili waweze kuchukua wanafunzi wengi katika kata hiyo iliyo na shule za Umma 5 pekee.

Pia amezishukuru sana Sos Children's Villages na na Taasisi ya Patel Brotherhood kwa kuendelea kushirikiana nao katika kuendeleza sekta za elimu na kuiomba serikali na wadau mbalimbali kuzidi kushirikiana ili kuipeleka sekta ya elimu mbali zaidi.
Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Ilala, Elizabeth Thomas akizungumza na wakati wa kukabidhiwa vyumba vya madarasa 11 katika shule ya msingi Chanika kutoka kwa Shirika la SOS Children Villages kwa kushirikiana na Taasisi ya Patel Brotherhood waliokarabati madarasa hayo.
Meneja mradi kutoka Shirika la  SOS Children Villages  Elamu Mkayange akizungumza kuhusu mradi wa kukarababti madarasa 11 ya shule ya Msingi Chanika pamoja na kutoa msaada wa Vitabu kwenye Shule zilizopo kata ya Chanika Jijini Dar es Salaam.
 Msemaji wa Taasisi ya Patel Brotherhood Anil Patel akizungumza kuhusu Taasisi yao inavyosaidia jamii lengo la kuinua sekta ya elimu na kuweka mazingira rafiki wa wanafunzi ili waweze kutimiza ndoto zao wakati wa kukabidhi madarasa 11 yaliyokarabatiwa.
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Chanika Ladislaus  Mutanda akizoma risala kwa mageni rasmi aliyemwakilisha Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala wakati wa wakati wa kukabidhiwa vyumba vya madarasa 11 katika shule ya msingi Chanika kutoka kwa Shirika la SOS Children Villages kwa kushirikiana na Taasisi ya Patel Brotherhood waliokarabati madarasa hayo.
Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Ilala, Elizabeth Thomas(wa pili kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa madarasa 11 ya shule ya Msingi Chanika yaliyokarabatiwa na Shirika la SOS Children Villages kwa kushirikiana na Taasisi ya Patel Brotherhood.

Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Ilala, Elizabeth Thomas  akimshukuru Msemaji wa Taasisi ya Patel Brotherhood Anil Patel mara baada ya kuzindua madarasa 11 ya shule ya Msingi Chanika yaliyokarabatiwa na Shirika la SOS Children Villages kwa kushirikiana na Taasisi ya Patel Brotherhood.
Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Ilala, Elizabeth Thomas akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kugawa vitabu kwa shule 10 zilizopo katika kata ya Chanika jijini Dar es Salaam vilidhaminiwa na Shirika la SOS Children Villages kwa kushirikiana na Taasisi ya Patel Brotherhood.
Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Ilala, Elizabeth Thomas akimkabidi mwanafunzi wa shule ya Msingi Chanika baadhi ya vitabu vya shule hiyo wakati wa zoezi la kugawa vitabu kwa shule takribani 10 zilizopo kwenye kata ya Chanika jijini Dar es Salaam.
Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Ilala, Elizabeth Thomas(katikati)  akimshukuru Meneja mradi kutoka Shirika la  SOS Children Villages  Elamu Mkayange(wa kwanza kushoro) kwa kuweza kutoa msaada wa vitabu pamoja ukarabati wa Madarasa 11 kwenye shule ya msingi Chanika jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Chanika wakiwa kwenye hafla ya uzinduzi wa vyumba vya madarasa 11 katika shule ya msingi Chanika vilivyokarabatiwa na Shirika la SOS Children Villages kwa kushirikiana na Taasisi ya Patel Brotherhood.


Baadhi  ya vitabu vilivyotolewa na  Shirika la SOS Children Villages kwa kushirikiana na Taasisi ya Patel Brotherhood kwa ajili ya Shule 10 zilizopo kata ya Chanika jijini Dar es Salaam.
 
 Baadhi ya madarasa ya Shule ya Msingi Chanika yaliyofanyiwa ukarabati na Shirika la SOS Children Villages kwa kushirikiana na Taasisi ya Patel Brotherhood.