Msanii wa muziki, muigizaji, na mjasiriamali Zuwena Mohammed maarufu kama "Shilole" amefunguka kuwa, ukiwa na mahusiano na mtu star huwa hakuna mapenzi.

Shilole ambaye yupo katika ndoa na mume wake Uchebe, kwa mwaka wa pili sasa, amesema hayo leo kupitia mahojiano na EATV na EARadio Digital.

"Inategemea mtu anataka mtu wa aina gani , kama mimi nilitaka mtu ambaye sio staa, ili niweze kuishi kwa raha, maana ukiwa na mahusiano na staa mtavimbiana , itakuwa sio sawa, hakuna mapenzi inakuwa mnaleteana maigizo".

Aidha msanii huyo amesema huwa anashika sana simu ya mume wake, na kama siku akikuta meseji ya msanii yeyote wa kike katika DM ya Uchebe atamtaja live. Pia ameweka wazi kuwa yeye na mume wake wanatumia simu moja kuingia kwenye mitandao ya kijamii kama Instagram.