BAADA ya ukimya wa muda mrefu bila kutoa ngoma mpya, mwanamuziki wa Dansi, Christian Bella ameibuka na kueleza sababu kuwa katika maisha yake hapendi kukurupuka kwenye kazi kwani anapenda akitoa wimbo uwe bora na siyo kubabaisha.  Akizungumza na Risasi Jumamosi, Bella alisema kuwa mashabiki zake wanalalamika kwa nini hatoi nyimbo wal a hafanyi shoo kama ilivyo kwa wasanii wengine lakini ukweli ni kwamba yeye huwa anafanya shoo zinazoeleweka na anakaa muda mrefu bila kutoa nyimbo kwa sababu anataka akitoa atoe wimbo unaoeleweka.

“Ukweli ni kwamba sikurupuki kutoa nyimbo wala sifanyi shoo za kuunga unga ndiyo maana niko kimya naangalia upepo ulivyo, pia mashabiki zangu wasitishwe na huu ukimya wangu kwa sababu kuna kitu kizuri nimewaandalia na ninaamini watakifurahia kwa sababu sijawahi kukosea hata siku moja,” alisema Bella