Waziri Muungano na Mazingira January Makamba pamoja na Naibu Waziri wa Maji Juma Aweso, wameshiriki ibada ya Kitaifa ya Sikukuu ya Eid ambayo kitaifa imefanyika mkoani Tanga, ambapo waumini mbalimbali wa Kiislamu wamejumuika pamoja.


Waumini wa dini wa Kiislamu wanasherehekea siku hiyo baada ya baada ya kuwa kwenye mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa kufunga kwa takribani siku 30.

Miongoni mwa mambo yaliyohimizwa kwenye ibada hiyo ni waislamu kuendelea kuyaenzi matendo waliyokua wakiyaishi kwenye mwezi wa mfungo pamoja na kupendana miongoni mwao na wasiokuwa waislamu.

Wakizungumza kwenye ibada hiyo January Makamba pamoja na Juma Aweso kila ameeleza kumshukuru Mufti Mkuu wa Tanzania Aboubakary Zubery kwa kuwaongeza vyema Baraza Kuu la Waislamu Tanzania