Mbunge Stanlaus Mabula amehoji juu magari ya polisi kutotengenezwa katika gereji za kisasa kama ilivyokuwa kwenye magari ya viongozi, huku akieleza mara nyingi polisi hao wamekuwa wakitegemea hisani ya Wabunge.


Mbunge Mabula ametoa kauli hiyo Bungeni jijini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali na majibu alipokuwa akiuliza swali la nyomngeza kwenda kwa Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi.

Swali

Mbunge Mabula aameuiliza kuwa : Mb. Mabula : Magari ya polisi yanategemea hisani ya Wabunge, nini mkakati wa Serikali?

Majibu ya Waziri

Naibu Waziri Masauni : Changamoto kubwa ni bajeti, wakati mwingine magari haya yanahitaji matengenezo makubwa ambayo yanahitaji fedha, niwapongeze wadau wanaojitokeza.