Na Stella Kalinga, Simiyu
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu amesema ni vema Sekreatarieti ya Maadili ya viongozi wa Umma iendelee kuwakumbusha viongozi na watumishi wa umma nchini kutimiza wajibu wao ili kuweza kufikia malengo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Serikali.

Mtaka ameyasema hayo Juni 03, 2019 Mjini Bariadi, wakati akifungua mafunzo kwa Viongozi wa Umma mkoani Simiyu, ambayo yameandaliwa na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora.

Amesema ikiwa kila mmoja katika Utumishi wa Umma atatimiza wajibu wake jamii na nchi kwa ujumla wake itaweza kufikia malengo yaliyowekwa na Serikali katika nyanja mbalimbali kwa wakati.

“Ni vizuri Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ikiendelea kuwakumbusha watu wote wanaofanya kazi zinazoihusu jamii kutimiza wajibu wao, kila mmoja akitimiza wajibu wake yapo mambo mengi sana sisi kama jamii, nchi, mkoa na kwa namna ambavyo uongozi na mgawanyiko wa .nchi yetu ulivyo tutafikia malengo yetu kwa wakati” alisema Mtaka.

Aidha, ametoa wito kwa viongozi wa Umma ambao ni watoa maamuzi katika maeneo yao ya kazi kuwa makini katika kutoa maamuzi na wahakikishe wanafanya maamuzi kwa wakati.

Kwa upande wake Kaimu Katibu Msaidizi Sekteratieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora, Bw. Gerald Mwaitebele amesema viongozi wa Umma wanapaswa kutoa maamuzi kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo iliyowekwa ili kutoiletea hasara Serikali.

Ameongeza kuwa Sekretarieti ya Maadili kwa Viongozi wa Umma itaendelea kutoa elimu kwa viongozi wa umma juu ya umuhimu wa kuzingatia misingi ya uadilifu katika uongozi na endapo ikitokea kiongozi yeyote atakengengeuka na kutofuata maadili sheria itachukua mkondo wake.

Kwa upande wake Hakimu mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Mary Mrio ameshukuru Sekretarieti ya Maadili kwa kutoa mafunzo ya maadili kwa viongozi wa Umma na akatoa wito kwa viongozi hao kuwa waadilifu, kutekeleza majukumu yao na kutojilimbikizia mali kinyume na taratibu na maadili ya viongozi wa Umma.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Bahame Kaliwa ametoa wito kwa Sekretarieti ya Maadili kwa viongozi wa Umma kutoa elimu ya maadili kila viongozi wapya wanapoteuliwa au kuchaguliwa, hususani madiwani wanapochaguliwa na kuunda Mabaraza mapya ya madiwani ili wajue misingiya uadilifu inayopaswa kuwaongoza katika kazi zao
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na Viongozi wa Umma mkoani humo, wakati akifungua mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora, ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi.
 Baadhi ya Viongozi wa Umma mkoani Simiyu wakifuatilia mafunzo yaliyoandaliwa kwa ajili yao na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora, ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi.
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akizungumza na viongozi wa Umma Mkoani humo, wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora, ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi.
 Kaimu Katibu Msaidizi Sekteratieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora, Bw. Gerald Mwaitebele, akizungumza na viongozi wa Umma Mkoani Simiyu, wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi hiyo, ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi.
 Afisa Maadili kutoka Sekteratieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora, Bw. Onesmo Msalangi akizungumza na viongozi wa Umma Mkoani Simiyu, wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi hiyo, ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi.
 Baadhi ya Viongozi wa Umma mkoani Simiyu wakifuatilia mafunzo yaliyoandaliwa kwa ajili yao na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora, ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi.
 Hakimu mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Mary Mrio akichangia hoja wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora kwa viongozi wa Umma Mkoani Simiyu, ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mhe. Robert Lweyo akichangia hoja wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora kwa viongozi wa Umma Mkoani Simiyu, ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi.