Shirika la Ndege nchini Rwanda, RwandAir limezindua ndege yake kuelekea kitovu cha biashara cha China Guangzhou, na kuifanya kuwa kituo cha 28 cha ndege hiyo kuenda.

Ndege RwandAir kuelekea uwanja wa ndege wa Kimataifa ya Baiyun Guangzhou itafanya safari zake mara tatu kwa wiki na Airbus A330 kupitia Mumbai, kwa mujibu wa viongozi wa RwandAir.

Guangzhou ni kitovu kikuu cha uagizaji wa bidhaa mbalimbali kuelekea Rwanda na njia mpya - ya kwanza kati ya mji wa China na Kigali ndege hii inatarajiwa kuongeza biashara na kurahisisha usafiri kati ya miji miwili.