Rubani mmoja ameaga dunia baada ya helikopta kuanguka juu ya paa la jengo moja refu sana huko Manhattan mjini New York nchini Marekani siku ya jana majira ya mchana.

Kulingana na taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari, ajali hiyo ilitokea karibia saa nane mchana kutokana na ukungu na mvua. Moto uliosababishwa na ajali hiyo uliweza kudhibitiwa kwa haraka.