Ikiwa yamepita masaa machache tu tangu msanii Jay Z atangazwe kuwa rapper wa kwanza kuwa bilionea, jarida la Forbes limemtaja msanii wa kike wa muziki Robyn Rihanna Fenty (Rihanna) kuwa msanii wa kike tajiri zaidi duniani


Jarida hilo limemtaja Rihana mwenye miaka 31 tu akitokea katika visiwa vya Barbados, kuwa na utajiri wa dola milioni mia sita ($ 600 m), akimzidi Madonna mwenye dola milioni 570, Celin Dion  dola milion 450 na Beyonce mwenye dola milioni 400.

Rihana ameweza kufikia hatua hiyo ya utajiri mkubwa duniani kutokana na bidhaa zake za urembo zimechukua nafasi kubwa katika kumuongezea mkwanja mrefu, pamoja na muziki wake.

Rihanna pia ni mmiliki mwenza wa The Savage X Fenty Lingerie, ambayo pia ni miongoni mwa biashara inayomuingizia pesa ndefu zaidi.