Real Madrid imeingia makubaliano ya kumsaini mshambuliaji Eden Hazard kwa dau ambalo huenda likapita £150m. Hazard amekubali kandarasi ya miaka mitano na atawasilishwa kama mchezaji wa Real Madrid tarehe 13 mwezi Juni baada ya kufanyiwa matibabu.

Mchezaji huyo wa Ubelgiji alifunga magoli 110 katika mechi 352 akiichezea Chelsea baada ya kujiunga kutoka lile ya Ufaransa 2012 na kufunga magoli mawili waliposhinda kombe la ligi ya Ulaya wiki iliopita.

''Kuondoka kwangu Chelsea ni uamuzi mkubwa na mgumu zaidi katika kipindi changu chote cha kucheza soka'', alisema Hazard.

MATANGAZO

Akiandika katika mtandao wa facebook aliongezea: Natumai munaelewa kwamba nililazimika kutafuta changamoto mpya kama vile inavyokua kawaida wakati mtu anapowania kuafikia ndoto yake.Kwa sasa ni wazi, nataka kuweka katika rekodi kitu kimoja kilichokuwa wazi kwangu, nimependa kila wakati wangu nilipokuwa chelsea na hakuna hata siku moja nilifikiria kwamba huenda nikahamia klabu nynegine.

Mkurugenzi wa Chelsea Marina Granovskaia alisema kumbukumbu anazotuwacha nazo hazitaangamia.

''Aliwafurahisha wote walioitazama Chelsea ikicheza na kwa hivyo tunamshukuru sana Eden Hazard. Amekuwa mtaalamu wa kuigwa katika kipindi chake chote akiichezea Chelsea , mtu mzuri kushirikiana naye na kufanya kazi naye''.

Katika misimu saba akiichezea Chelsea Hazard ambaye kandarasi yake katika klabu ya Chelsea ilikuwa inakaribia kukamilika baada ya mwaka mmoja alishinda kömbe la ligi na lile la Ulaya mara mbili kömbe la FA na lila la Ligi.

Pia alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa Chelsea mara nne.

''Ijapokuwa ni uchungu sana kumwambia kwaheri Hazard licha ya klabu kumtaka kusalia , tunaheshimu uamuzi wake wa kuchukua changamoto mpya katika taifa tofauti na kufuata ndoto yake ya utotoni kuichezea Real Madrid'', aliongezea Granovskaia.

Chelsea itahudumia marufuku ya uhamisho , ikimaanisha kwamba hawataweza kumsaini mchezaji mwengine atakayechukua mahala pake Eden Hazard hadi mwisho wa Januari 2020.

Walishindwa katika rufaa yao ya kwanza na sasa wamewasilisha rufaa yao ya pili katica mahakama ya michezo inayotatua mizozo.