Baada ya mchana wa June 13 2019 kutangazwa kuwa club ya Real Madrid imemfanyia vipimo vya afya Eden Hazard na kumtambulisha kwa uongozi, ilifika wakati wa mashabiki wa Real Madrid kupata fursa ya kumuona staa huyo akitambulishwa.

Real Madrid indaiwa kuwa wamemleta Hazard kutoka Chelsea kutokana na kutafuta jina kubwa linaloweza kuungana nao kuziba jina la Ronaldo, kwa kifupi Real Madrid ambao wamemtambulisha Hazard mbele ya mashabiki elfu 50000 katika uwanja wa Santiago Bernabeu, walikuwa wanahitaji staa mpya wa timu yao.