Inaelezwa kuwa Filamu ya “Surviving R Kelly” iliyoachiwa rasmi January 3,2019  ya mkongwe wa muziki wa RnB Robert Kelly imeshinda tuzo ya “Best Documentary” kwenye tuzo za filamu za MTV za mwaka huu wa 2019 nchini Marekani.

Filamu hiyo ambayo iliibua maovu mengi ya mwimbaji huyo na kuchafua kazi yake ya muziki na kuibuka kwa tuhuma za unyanyasaji wa kingono kwa wanawake 10 waliokuwa chini ya umri wa miaka 18 ambapo R. Kelly alikanusha tuhuma hizo na kusema kuwa hazikua na ukweli wowote inatajwa kuangaliwa na watazamaji zaidi ya Mil.22 katika mtandao wa You Tube.

Inaripotiwa hadi sasa nguli huyo amefunguliwa mashtaka zaidi ya 11 ya unyanyasaji wa kingono pamoja na kuwekwa gerezani mara mbili huku ikielezwa kuwa watu wengi wamejifunza vitu vingi kupitia filamu hiyo ya ‘Surviving R Kelly”