MWANAMUZIKI wa marekani R. Kelly ameendelea kukana mashtaka yanayomkabili dhidi ya tuhuma za unyanyasaji wa kingono kwa mabinti. R. Kelly amekana mashtaka yote 11 dhidi yake yaliyofunguliwa mwishoni mwa mwezi Mei mwaka huu.

R.kelly alipandishwa kizimbani kwenye Mahakama ya Cook mjini Chicago kujibu mashtaka hayo 11 ambayo manne yamepewa daraja X ambayo yanatafsiriwa kama makosa ya jinai na huenda yakampeleka jela mika 30 endapo atakutwa na hatia.