Msanii wa Muziki, Queen Darleen amesema kuwa kama mpezi wa Diamond, Tanasha ana mimba watajua tu kwasababu mimba inaenda mbele hairudi nyuma.

Darleen amesema kuwa hata yenye alivyoona alishtuka na kuuliza jamani vipi hapa?  huku akisema kama ni mimba Mwenyezi Mungu amsaidie ajifungue salama wapate Aunty.

"Kama ni mimba, mimba hairudi nyuma inaenda mbele tutaona tusubirie Inshaallah kwasababu mimi mweyewe nilivyoona nilishtuka eeh jamani vipi hapo kwahiyo kama ni mimba tutaona tu siinakuja mbele hivi labda iingie kwenye maziwa kwasababu wengine wanasema zinaingiaga kwenye maziwa," Darleen ameiambia SnS.

"Kwasabubu yule ni mwembamba unaona kama kweli ni mimba na sisi Inshallah tunaomba heri Mwenyezi Mungu amjaalie aweze kujifungua salama tumuone kama auncle au aunty yetu kama ni mimba namini hata ndoa inshaallah Mungu atajaalia."

Mitandaoni watu wamekuwa wakijadili kuwa mrembo huyo kutoka nchini Kenya huenda akawa ni Mjamzito kutokana na clip ya video waliyoitoa wakicheza na Diamond wimbo wake mpya.