MREMBO ambaye alijizolea umaarufu hivi karibuni baada umbo lake kuonekana kuwavutia watu mbalimbali Bongo, Jacqueline obeid ‘Poshy’ amewataja wanawake kama ndiyo watu wanaoongoza kwa chuki na roho mbaya na sio wanaume.Poshy aliiambia Za Motomoto kuwa amegundua kuna wanawake wengi hawapendi kuona wenzao wanaendelea hivyo wataweka kila aina ya chokochoko ili kutibua.“Watu tu wanashindwa kuelewa kuwa huku duniani kila mtu ana bahati yake hivyo ukiona mwenzako anafanikiwa au mwanamke mwenzako anafanya vizuri mshike mkono uzidi kumfanya ainuke ili akuinue na wewe na sio kumponda kila kukicha maana huo unaitwa wivu,” alisema Poshy ambaye tayari amejikwamua kwa kufungua duka lake la kuuza nguo za ndani.