Siku chache baada ya picha zake kusambaa akionekana na wabunge tofauti kwenye Viwanja vya Bunge jijini Dodoma, huku kukiwa na madai kuwa ameenda kudanga, mrembo anayetikisa na umbo matata katika mitandao ya kijamii, Jacqueline Obeid ‘Poshy Queen’ amevunja ukimya juu ya safari yake hiyo.

Poshy amesema kuwa anawashangaa sana watu wote wanaomjadili na kumsemea maneno mabaya na kuuliza kuwa  yeye kwenda bungeni ni makosa.

"Mbona watu wana matatizo sana, yaani mimi kwenda bungeni ni matatizo jamani au sistahili? Kule kila mtu anakaribishwa kama mgeni wakati mimi kuna jambo lilinipeleka kule na nimejifunza vingi", amesema Poshy.

Poshy ameongeza kuwa asingependa kabisa watu waendelee kumjadili kuhusu yeye kwenda bungeni kwa sababu kila mtu anaruhusiwa kwenda, lakini alivyokwenda yeye ilikuwa kwa sababu maalum ya kipindi cha Bunge la Bajeti ambapo amesomea mambo ya usimamizi wa fedha katika Chuo cha IFM jijini Dar es salaam.

“Kule nilikwenda na mimi kuwasilisha mawazo yangu katika kipindi hiki cha Bunge la Bajeti, licha ya kuhudhuria hata nilivyokutana na baadhi ya wabunge niliwaambia mawazo yangu na wamesema watayafikisha huko", ameongeza Poshy.

Katika habari zilizoenea, Poshy alidaiwa kuwa alikwenda jijini humo kudanga baada ya kupata mualiko na mbunge mmoja ambaye ana uhusiano naye. Poshy ametokea kujizolea umaarufu mitandaoni kutokana na umbo lake matata la namba nane ambalo inasemekana kuwa amelipata ghafla au ni la kutengeneza.